Rapper Kalapina mmoja kati ya wadau ambao walimsaidia Chidi Benz kumpeleka Sober House amefunguka kwa kusema kuwa kitendo cha Chidi Benz kukatisha muda wa matibabu akiwa Sober House kumemkosesha vitu vingi pamoja na kupelekwa Ulaya kwa ajili ya matibabu.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumanne hii, Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka ‘sober house’.

“Chid Benz hakumaliza muda wa matibabu alivyotoka ‘sober house’ ndani ya siku 28, kwahiyo mi namuomba afikirie faida alizozipata sober na faida anazozipata sasa hivi akiwa mtaani, nafasi bado ipo kwake kwa sababu tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa, kwa hiyo anatakiwa atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza kujisahihisha”, alisema Kalapina.

Kalapina amesema Chidi Benz alipata wafadhili wa kumpeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kitendo hicho.

“Kulikuwa kuna safari ya yeye na Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa matibabu zaidi, lakini ilitakiwa subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka kukaa sober anataka kukaa mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena ku’invest hela yao inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com