Hakuna asiyejua aina ya muziki anaoufanya Nay wa Mitego. Ni muziki flani hivi ambao huwa unaongea na wale ambao Nay anawaona kuwa wameenda wrong. Na hivyo Nay wa Mitego huwa anawachana kupitia nyimbo zake.
Wapo wakerekwa wengi wa nyimbo za mkali huyo, na pia mara kibao tumesikia zikimletea matatizo hadi kufikia hatua ya kuvunjiwa kioo cha gari na vitu kama hivyo. Na ndio sababu ya wasanii wengi wakubwa kuogopa kufanya collabo na mkali huyo kwa kuogopa kuonekana mshiriki kwenye ngoma ambayo imemzungumzia mtu fulani vibaya.
Imetokea mara kibao kwa chorus killer Belle 9 kupigiwa simu na msanii Nay wa Mitego kutaka kushirikishwa katika nyimbo zake lakini Belle 9 amekuwa akimkimbia Nay kila mara.
Sasa leo wote wawili wamekutana na kipaza cha Perfect255 na kila mmoja anafunguka yakwake kuhusiana na issue hiyo.
“Nay wa Mitego kwenye ngoma zake anavyo wachanaga watu yani huwa ni moja kwa moja anamaanisha yan. ndio maana mimi huwa namkimbia ili kuepuka lawama.” Ni baadhi ya maneno ya Belle 9, huku Nay wa Mitego akidai kuwa hawezi kumlaumu kwasababu yeye mwenyewe anajua aina ya muziki ambao anaufanya.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com