Barnaba amedai kuwa awali Ruby aliukataa wimbo ‘Na Yule’ alioundika.

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, mwandishi huyo mahiri wa nyimbo alisema aliitwa amuandikie wimbo msanii huyo.

“Nikaandika nyimbo tatu lakini for the first time nikamuambia imba huu, ule wimbo nilimwandikia Ruby na kuucompose then Tudy akaja kufanya mastering kumalizia finishing,” alisema Barnaba.

“Lakini nilivyompa akakataa alisema ‘huu wimbo unasound kigospel sana.”

“Lakini baadaye kipindi nimeenda out sasa akaanza kunipigia simu sasa kuniambia ‘I can’t believe it’ ambavyo anapokea mrejesho kwa watu.”

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com