Mimi ni mpenzi mkubwa wa muziki na hasa muziki wa dansi ingawa nyimbo nyingi sizijui. Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kuwasikiliza Washirika Tanzania stars na mpaka sasa nikisikia nyimbo yao yoyote natulia kwa makini kusikiliza. Hiyo ilikuwa bendi pendwa kwangu kabla hawajasambaratika na kujikuta nikitekwa na wakongo hasa hasa Wenge Musica BCBG na kidogo ikaingia Nouvelle Generation.

Waliposambaratika hao nilijikuta katika majonzi baadae nikapata faraja kwenye nyimbo za dini. Bado nafuatilia muziki ila si kwa nguvu ile tena, itokee tu (in sheikh Kipozeo tone).

Niingie kwenye mada. Muziki wa Tanzania umekuwa kwa kiasi kikubwa na unapozungumzia mastaa wanaotamba vilivyo utawakuta Ali Kiba na Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz. Watu hawa wamejijengea umaarufu mkubwa na kujitengenezea mashabiki ambao wamegeuka mahasimu wakubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa instagram.

Mimi binafsi si shabiki wa mtu yoyote kati ya hao ila kuja mmoja akitoa wimbo wake (hit song) najikutaga nafuatilia mwenendo wake kwa mashabiki na vyombo vya habari. Kimsingi Alikiba alivuma sana kabla ya Diamond na alifanikiwa kufanya show nyingi nje ya nchi hususan Uingereza na Marekani ambapo nahisi ilikuwa mwanzo wake wa kuporomoka kimziki kabla hajaamshwa na watu wanaomchukia Diamond na kumtengeneza kama mtu atakayemshusha Diamond kimuziki.

Alikiba amesahau kazi yake kama mwanamziki amejikuta kwenye harakati za kupambana kumshusha mwenzake ili akae kileleni. Hii itaugharimu muziki wa Tizii kwani kushuka kwa Diamond hakutamuweka Ali Kiba juu kivile kwa kuwa hajui kukaa kileleni. Katika harakati zake za kumshusha Diamond kileleni amejikuta yeye na timu yake wakijaribu ku counter pale Diamond anapoachia hit song mpya.

Kitu kilichonisukuma kuandika huu uzi ni baada ya Diamond kuachia wimbo wake wa Salome ambao ni remix ya wimbo Maria Salome wa Saida Karoli. Siku moja baada ya kuachia wimbo huo Alikiba naye akaachia wimbo wake wa Nitulize. Nimezisikiliza nyimbo zote mbili kwa kiasi ila nimefuatilia ni kwa kiasi gani nyimbo hizo zimepokelewa na mashabiki na kugundua Alikiba amefanya Tuming mbaya sana.

Ni afadhali angeacha Salome akakaa hewani kwa wiki moja au mbili ili atoe yake. Sio uongo kuwa Diamond ana mashabiki wengi across the continent na hayo yanathibitishwa na kauli ya wanamuziki wenzake wa Afrika kama akina Mafikizolo na Davido. Labda niongee kidogo, Jumatatu nilikuwa niko bored nyumbani na wife hayupo kaenda msibani nikawa naangalia chanel hazinivutii baadae nikajikuta nimeweka chanel E.

Hapo nilikuta Mafikizolo wakiwa wanahojiwa walivyomtafuta Davido. Baada ya kumpata Davido ili wafanye collabo aliwaambia pia wamtafute Diamond kwani ni mtu mwenye mvuto kimuziki na ana mashabiki wengi ambapo kila msanii wa Afrika anatamani kuwa kama Diamond. Hiyo testimony inanipa fursa ya kusema Diamond yuko mbali sana kimuziki kuliko Alikiba.

Mwisho nakuomba msomaji uangalie youtube mapokezi ya Salome na Nitulize halafu uniambie nani anafanya vizuri. Alikiba alipofanya vizuri alirudi kulala na kushtuka underground wake kawa leader wake. Akitaka kufanikiwa ajiwekee malengo ya kutoka alipo kusogea mbele na si kumkimbiza mtu.

Na pili akumbuke yeye yuko chini ya lebo ya watu wengine ( sony) wakati mwenzake anafanya muziki chini ya lebo yake mwenyewe kwa hiyo sijui kama hiyo itamtengenezea wigo wa kuwa na lebo yake kama anavyojaribu kufanya kwa kuwachukua baadhi ya wanamuziki kama Baraka da Prince kuwa ndani yake.

Imeandikwa na Kingwipa1

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com