Mziki wa bongo fleva umepata umaarufu mkubwa sana Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Kitendo hiki cha mziki wetu kuvuka border kimesaidia sana kuongeza Ajira kwa vijana na kukuza vipato vya wasanii wetu.

Miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri ni Alikiba na Diamond. Wasanii hawa wawili wamejikita zaidi kuutangaza mziki wetu kimataifa hivyo kujipatia umaarufu mkubwa sana. Na kama tunavyojua Umaarufu ni moja kati ya vitu vitakavyokufanya upate pesa kwa uraisi zaidi.

Msanii Diamond platnumz amejikita zaidi kuwekeza katika Ardhi kama anavyosema mwenyewe "Najenga vibanda" na mpaka sasa ana vibanda zaidi ya viwili vimesimama kama "Kangaroo"
Kwa upande wa kiba bado sijajua anamiliki Vibanda vingapi ila najua ancho hata kama ni kimoja ila tu hapendi kujionesha. Hivi majuzi tulipata tetesi ya kuwa anataka kununua gari yenye thamani ya M700 na pia anataka kununua Helikopta kwaajili ya kumfikisha hapa na pale huku Hasimu wake nae inasemekana anataka kununua Boti.

Show ya mwisho kufanya Diamond alilipwa M5 za kenya na kiba alipata M3 hii inaonesha mmoja wao ana gharama zaidi kuliko mwenzake.

Binafsi nawapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com