Miezi michache iliyopita Abdul Kiba ambaye ni mdogo wake na AliKiba alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari kwamba yupo tayari kujiunga na label ya ‘WCB’ ya Diamond kauli ambayo ilileta shida kwa mashabiki wa AliKiba pamoja na team yake.
Ali Kiba na Abdul Kiba
Ali Kiba na Abdul Kiba
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Bayoyo’ ameiambia Bongo5 kuwa kauli hiyo ilimfanya aonekane msaliti.
“AliKiba akijisikia vibaya kwa sababu alijua kama ndo vile tena ndugu yake nimekuwa msaliti kumbe ni watu walipata definition nyingine na ni kitu ambacho hakiwezekani ila niliweza kufanya interviews nikaweka mambo sawa,” alisema Abdul Kiba.
Akifafanua kauli yake aliyozungumza na kutafsiriwa vibaya Abdul Kiba alisema “Siku ambayo nilifanya interview walinielewa vibaya maongezi yangu, unajua unaposikia kwamba kuna kazi hakuna kazi ya bure, kazi yoyote lazima iwe na malipo, nilikubali kwamba kama WCB watanihitaji kwa kolabo au show naweza nikajoin nao kufanya kazi ila sikutoa kauli kwamba naweza kwenda label yao kwa sababu hata mimi na label yangu,”
Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa team Kiba kwa kuendelea kuwasapoti wasanii wake pamoja na kazi zao.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com