diaspora
Serikali imesema ina mpango wa kuandaa Sera ya Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora Policy), itakayoainisha namna ya kuwapunguzia masharti  Watanzania waliobadilisha uraia wao ili waweze kuja kuwekeza na kufanya kazi nchini bila vikwazo.
Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la tatu la Diaspora linalotarajia kuanza leo visiwani Zanzibar.
Na akasema kwamba kwa vile mpaka hivi sasa Tanhzania haijaruhusu uraia wa nchi mbili, sera hiyo itasaidia kuainisha maeneo ambayo yanaweza kuondolewa vikwazo kwa Watanzania waliobadilisha uraia. ili kuwaruhusu waje kufanya kazi kwa kipindi fulani bila kuwekewa masharti wanayowekewa wageni wengine ambao si watanzania wanaofanya kazi kwa kibali.
Licha ya kuwaruhusu kufanya kazi bila masharti, vile vile wanaweza kuruhusiwa kumiliki ardhi kwa kipindi ambacho watakuwa nchini. Yote hii ikiwa ni kama sababu ya kuwahamasisha  zaidi kuja kufanya kazi na kuwekeza nchini tofauti na ilivyo sasa.
Akizungumzia kuhusu ugumu wa kuruhusu mtu kuwa na uraia miwili tofauti, alisema suala hilo linatakiwa kupitishwa na Bunge, na kwamba hoja iliyopo ni kuhusu usalama wa nchi endapo suala hilo litaruhusiwa.
Alisema kupitia Idara ya Diaspora wanaendelea na jitihada za kuwatambua Watanzania waishio nje na umuhimu wao kwa taifa, ili kuonyesha faida za kuwa na uraia wa nchi mbili.


0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com