black-couple-marriage-750x375
black-couple-marriage-750x375
Wakati mwanaume anapofikia kuona, huhitaji kutafuta mke na sio mpenzi wa kike. Lakini utawezaje kujua tofauti yao? na hii ina umuhimu gani?
Hii ni muhimu sana kwa sababu mpenzi wa kike yeye anataka kukaa na wewe kwa ajili ya burudani tu. Wanadhani mambo kama kuwa mwaminifu ni vitu vya kishamba na huwa hawana mpango wa kuolewa karibuni sababu wao ni kula bata tu ndicho wanachowaza.
Jambo jema ni kuwa ni rahisi sana kuweza kujua huyu anafaa kuwa mke na huyu mpenzi wa kike, mfano tu wakitoka, nguo anazovaa na urembo anaojiwekea. Hivyo kama unataka kuoa, tafuta mwanamke anayevaa nguo za kujisitiri.

Mpenzi wa kike anaweza kucheza usiku mzima na anakunywa chochote kinachopita mbele yake na hawezi kuwa mwaminifu, kwanza kwanini awe mwaminifu wakati ukimuacha anapata mwingine na maisha yake yanaendelea? hayo anaona ni mambo ya baadae sana, atajigongesha kwa marafiki zako na atakayeonyesha nia basi anakwenda nae.
Mpenzi wa kike anategema mpenzi wake wa kiume ajue namna anavyojisikia hivyo watakuwa wanafanya visa lakini mwanamke anayefanaa kuwa mke ataelewa kwamba hapa mwanaume hataelewa hivyo yupo tayari kumwambia anachowaza.
Mpenzi wako wa kike anatarajia gharama za mambo yote zitakuwa juu yako, lakini mwanamke ambaye tayari anataka kuwa mke na yeye ataonyesha ushirikiano na hii itakusaidia kukuonyesha kuwa huyu tunaweza kufanya jambo kwa pamoja kama timu.
Mpenzi wa kike huwa ni vigumu sana kumfurahisha, kila mara atakuja na kioja kipya. Kila mara hubadilisha status zao za Facebook au mitandao mingine. Hivyo chagua mwanamke ambaye hana mambo hayo na anakuwa Facebook anapokuwa amemaliza mambo yake au kuna jambo la muhimu.
Vipindi anavyoangalia kwenye Tv ni vya kiumbea umbea na hua anapenda kuongelea watu na tamthilia. Mwanamke anayefaa kuwa mke sio kwamba yeye haangalii lakini hupata wasaaa wa kufanya mambo mengine kama kujisomea, atakuwa akifanya majibizano yenye mantiki na watu ambao anaamini watamsaidia na kukuza uelewa wake.

Mpenzi wa kike ukienda naye out utaona vile vitu anaangiza, yeye hula vitu ambavyo hata hajui majina yake lakini tu ili aonekane wa kisasa. Unahitaji mwanamke ambaye yupo tayari kukaa chini na wewe na kula kile ambacho ni size yenu, ambaye hahitaji kuigiza kwenye maisha.
Tafuta mwanamke ambaye yupo tayari kutumia fedha kwa ajili ya chakula cha familia na siyo anayenunua kila fasheni inayotoka. Anayeweza kukaa chini na kulea watoto na kuitunza familia, atakayekuwa mwaminifu kwako. Huyo atakufanya uwe mwenye furaha.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com