Mwimbaji wa bongo fleva Kassim Mganga amefunguka na kusema kuwa maisha mengi ya wasanii wa muziki huo hayako kama vile wanavyoonyesha kwenye mitandao.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa,Kassim amedai watu wasanii wengi huiga wasanii wa nje kuonyesha maisha ya kifahari bila kujua kuwa wenzao ndio maisha yao ya uhalisia hivyo ni kama wanadanganya mashabiki.
Kitu ambacho nimejifunza, wenzetu hawa’act, wenzetu wako real, ndio maisha yako vile, ukimuona Chris Brown au ukimuona 50 Cent pamoja na umri wake aliokuwa nao leo, anaonesha magari yake,ni kwa sababu watu wapo kwenye ushindani wa biashara kubwa sana, kwa hiyo anachokifanya kina mantiki, sisi tumekuwa tuna’fake vitu vingi havipo real, lakini tunataka tuwaoneshe kwenye mitandao, tunadanganya, tunawadanganya sana mashabiki wetu, mashabiki wanatuona si watu ambao tuna maisha makubwa sana, wakati haiko hivyo kiuhalisia“, alisema Kassim Mganga.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com