Msanii wa bongo fleva,Dullayo ambaye amewahi kutamba na vibao vyake kama naumia roho na mida ya kazi amelalamikiwa na majirani kwa kukithiri kwenye tabia ya ulevi.
Wakiongea kwenye kipengele cha Cheche kinachopatikana kwenye kipindi cha E-Newz cha East Africa TV kinachozungumzia maisha ya mastaa wakiwa mtaani,majirani hao ambao wengi walimsifu Dullayo kwa kutokuwa na maringo kama mastaa wengine walisema tatizo la msanii huyo ni Ulevi.
Kusema kweli Dullayo ni msanii mzuri,mdogo wetu,tunaishi naye vizuri katika mtaa wetu lakini kitu kimoja Dullayo anatuudhi anakunywa sana pombe na msanii anapokunywa saana pombe badaye anakuja anaharibika” alifunguka mwanadada mmoja wa mtaani kwa msanii huyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com