Kwa hili linalotokea kwa Diamond kwa sasa ni kama kero kwa baadhi ya watu lakini ni sherehe kwa upande wa mashabiki wake kutokana na kila siku anaibuka na stori mpya na kubwa ambazo zinateka vichwa vya habari.

Baada ya hapo jana stori ya kumpatia zawadi ya gari Raymond kukiki, leo yameibuka mapya na makubwa zaidi baada ya hitmaker huyo wa Kidogo kuonekana akiwa na staa wa Nigeria, Wizkid huku mashabiki wakijiuliza nini kinaendelea?

Vipande viwili vya video alivyopost Diamond kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na staa huyo wa Nigeria vimewashtua mashabiki kutokana na hitmaker huyo wa ‘Shaba’ kwa sasa siyo msanii wa kitoto kwa kuwa muziki wake tayari tayari umepenya nchini Marekani na tayari ameshafanikiwa kufanya collabo na mastaa wa nchi hiyo akiwemo Swizz Beat, Drake na Chris Brown.


Haikuwa ngumu kwa hitmaker wa ‘Kidogo’ kukutana na staa huyo kutokana tayari wameshakutana mara kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya show kwenye jukwaa moja ikiwemo ile ya ‘One Africa’ iliyofanyika nchini Marekani mwezi uliopita pamoja na ile iliyofanyika nchini mwaka jana kwenye viwanja vya Leaders Club.

Hata hivyo inadaiwa kuwa vipande hivyo vya video vinavyowaonyesha wasanii hao walikutana Afrika Kusini na siyo Bongo kama watu wanavyofikiria kwakuwa huenda Wizkid aliondoka Dar August 22.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com