Msanii wa bongo fleva,Bonge la Nyau amefunguka na kusema kufanya kazi na Ali Kiba kumempandisha kiwango na kufanya watu wengi kumfahamu tofauti na awali.
Akiongea kwenye kipindi cha 5 selekt cha East Africa amedai kuwa wimbo wake wa Uaminifu alioufanya na Kiba ndio wimbo wake uliotazamwa kuliko nyimbo zake zote kwenye youtube na ndio wimbo unaobamba akifanya show.
Nimefanya nyimbo nyingi lakini kiukweli mpaka sasa wimbo niliofanya na Ali kiba nauheshimu sana moja kwa sababu ni wimbo ambao umeangaliwa sana ‘Youtube’ kuliko nyimbo zangu nyingine, lakini pia ni wimbo ambao nikipanda stejini kuimba naimba na mashabiki mwanzo mwisho, sababu wanaifahamu vyema hivyo wimbo ule kwangu ni mkubwa sana“. Alisema Bonge la nyau

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com