Msanii wa bongo fleva,Barnaba amedai kuwa nywele ni moja kati ya vitu anavyovipenda sana kwenye mwili wake.
Akiongea kwenye moja ya mahojiano yake na Times Fm,Barnaba ambaye anafuga rasta amesema kuwa analazimika kwenda saloon kila baada ya siku tatu kuweka sawa nywele zake,hivyo hutumia kiasi kikubwa cha pesa kwenye nywele zake.
Natumia pesa sana kutengeneza nywele zangu, kila baada ya siku tatu lazima nipite saloon kwa ajili ya kuzirekebisha, unajua dawa zake ni bei na kuzifanya ziwe nyeusi zaidi ni gharama pia” alisema Barnaba.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com