Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Afrika Radio, Kayumba amesema pesa bado ipo ingawa imeshapungua, tofauti na alivyosema Mkubwa Fela, na kwamba hata ujenzi wa nyumba bado unaendelea.

“Hela ipo, ingawa sio tena milioni 50 , itakuwa uwongo nikisema bado ipo milioni 50, lakini zipo siwezi kusema imebakia ngapi, si unaona napendeza nini, nyumba ipo kama nyumba zingine, kawaida siwezi kuzungumzia labda vyumba vingapi, ili mradi nitaweka ubavu wangu nitashukuru Mungu”, alisema Kayumba.

Hivi Karibuni kulikuwa na tetesi ambazo zilipigiwa mstari na bosi wa msanii huyo Mkubwa Fela, kwamba pesa alizoshinda msanii huyo zilishaisha kitambo, na nyumba yake ya kuishi ikiwa bado haijakamilika.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com