Young Dee akiwa na boss wake, Max Rioba
Uongozi wa label ya Millian Dollar Boys ‘MDB’ unaomsimamia rapper Young Dee, umesema rapper huyo tayari amesharekodi ngoma 200 mpya ambazo zinasubiria kutoka.

Akiongea na waandishi wa habari Jumatano hii, Mkurugenzi wa label hiyo, Max Rioba, amesema Young Dee ana ngoma ambazo zikitoka zitabadili taswira ya muziki wa bongo.

Wimbo mpya anaofuata sasa hivi unaenda kutengeneza historia mpya katika tasnia ya muziki,” alisema Max.

Aliongeza, “Kuna kitu kingine hamjui, Young Dee ana nyimbo zaidi ya mia mbili ambazo tunazo studio, kwa mfano juzi kati tulipost kavideo fulani akiimba, hiyo ni moja kati nyimbo mia mbili na kitu,”

Rapper huyo ambaye siku hiyo alikiri kutumia Madawa ya kulevya, aliwaomba radhi mashabiki wake huku akiwaahidi mambo mazuri kutoka kwake.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com