Msanii mdogo mwenye mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya muda mchache amekanusha habari zinazosambazwa na watu wasiompenda kwamba amekamatwa na poliisi. Akitolea maelezo suala hilo kutoka kwenye nyumba yake anayomiliki maeneo ya Sinza alidai kwamba hajakamatwa na mtu yeyote yule ila alikuwa akishoot video ya wimbo wake mpya unaoitwa "Jirani nitakuvunjia simu yako" ambapo director alishauri simu ivunjwe ili kuleta uhalisia ."Unajua director alikuwa too authentic,hata sisi ilibidi tuvunje simu ya jirani"

Pia Young D ametolea ufafanuzi suala la madawa kulevya na kusema yeye angekuwa anatumia madawa ya kulevya asingekuwa anafukuzana kwenye chati na Diamond na Wizkid hapa Afrika pia kuweza kumiliki mtoto mkali Afrika Mashariki .

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com