Ikiwa ni siku tatu zimepita tangu mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kusimama bungeni na kuomba mwongozo wa spika kuhusu kitendo cha kuvuliwa kofia ‘baraghashia’ na mbunge wa viti maalum CHADEMA Anatropia Theonest. Naibu spika Dk. Ackson Tulia kalitolea ufafanuzi baada ya kupitia CCTV camera za bunge .

Dk. Tulia alisema…
’Mbunge Goodluck Mlinga katika mwongozo wake alilalamikia kitendo cha mbunge Anatropia kumvua baraghashia aliyokuwa amevaa siku hiyo, kitendo kilichomfanya asiwe na sifa ya kukaa ndani ya bunge kama sheria inavyosema‘ –Dk. Tulia Ackson

‘Nimepitia picha za video za siku hiyo na nimejiridhisha ni kweli baada ya kusomwa dua wabunge wa kambi ya upinzani walianza kutoka nje ya bunge na mbunge Anatropia alipita sehemu aliyokaa Goodluck na kumvua kofia aliyokuwa amevaa na kisha kutokanayo nje ya bunge‘ –Dk. Tulia Ackson

‘Kitendo hicho kilikuwa cha kudharau kiti cha spika pia kilikuwa kitendo cha fujo ndani ya ukumbi wabunge, nachukua hatua ya kutoa onyo kali kwa mbunge Anatropia kwamba kitendo alichokifanyi ni ukiukwaji wa sheria za bunge na endapo atarudia sheria mahususi zitachukuliwa‘ –Dk. Tulia Ackson

Full video nimekusogezea hapa chini unaweza kuitazama...

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com