Aliyekuwa meneja wa wasanii walikuwa kwenye kampuni ya Endless Fame chini ya Wema Sepetu,PetitMan amesema kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye kampuni hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia lakini hata tatizo na Wema Sepetu na kuwa wanaongea kama kawaida.

‘’Endless Fame nilikuwa kama ‘Coordinator’ na pia nilikuwa meneja wa wasanii, kwa sasa hivi nimesimama kufanya kazi Endless kutokana na matatizo yetu ya kifamilia na unajua ile kampuni ni kama familia yangu nimekaa nayo kwa miaka tisa, nimeishi na Wema Sepetu zaidi ya miaka tisa kwahiyo siwezi kusema kitu chochote kwenye media kwa sababu sina tatizo na Wema wala Martin Kadinda, matatizo yametokea upande mwingine, kuna tofauti ilitokea kati yangu mimi na Mirror lakini sasa hivi tuko poa’’ Alisema PetitMan akiwa kwenye kipindi cha Leo Tena.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com