Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Serikali yasistisha ajira zote’
 Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake
Gazeti hilo la Mtanzania limeripoti kuwa Serikali imesitisha ajira zote kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa. Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali vya likizo ya bila malipo.
Gazeti hilo limezungumza na Katibu Mkuu utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro ambaye amesema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.
Aidha Dk. Ndubaro alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi.
>>>‘Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki

Aliongeza pia muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya mishahara, hivyo ni lazima ujue nani unayemlipa kuliko hivi sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com