Msanii wa muziki wa Hip hop ambaye siku zote amekuwa ni mtunzi wa nyimbo zinazogusa maisha ya watu kiasi cha kuitwa mwanamuziki mkosoaji Kala Jeremiah amesema kuwa Rais Magufuli alianza na kasi nzuri ambayo ilileta matumaini kwa watu wengi lakini saizi anaona kama kasi yake inakwenda ndivyo sivyo.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Kala Jeremiah alidai kuwa hata yeye alikuwa ni mtu ambaye alifurahishwa na kasi ya Rais Magufuli na alionyesha hisia zake wazi wazi toka mwanzo, lakini anakatishwa tamaa na kitendo cha kuzuiwa kwa bunge na kusema hilo pekee linaweza kuondoa sifa nzuri na kasi ambayo Rais alianza nayo kama ile ya kutumbua majipu.

"Kiukweli kabisa Rais alianza na kasi nzuri sana, mfano sisi kila siku kwenye nyimbo zetu tulikuwa tunaimba juu ya matatizo ya ufisadi ambayo yeye alianza nayo kwa kutumbua majipu, hivyo hata sisi tulikuwa tunatumbua majipu hayo hayo. Lakini nadhani kwenye suala la bunge live aingilie kati la sivyo kwenye Serikali hii tutakuwa nyimbo nyingi sana za kuimba kuliko muda wote" alisema Kala Jeremiah

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com