MSANII anayekimbiza katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Quick Rocka amedai kuwa penzi la muuza sura kwenye Filamu za Kibongo, Kajala Masanja halimtesi maana ni la kishkaji na kila mmoja kati yao ana uhuru wa kufanya mambo yake binafsi kutokana na matakwa yake bila kumbana mwenziye.

Akipiga stori na safu hii ya burudani Quick ambaye kwa sasa ameachia ngoma mpya iitwayo Hapo aliyomshirikisha G Nako alisema, tofauti na watu wengi waliyoko kwenye mapenzi wanaokuwa wanabanwa na wapenzi wao katika shughuli za kawaida kwa ajili ya kujitafutia kipato, kwake haiko hivyo, yeye na Kajala wamepeana uhuru.

“Sijui nikweleze vipi kuhusu penzi langu na huyo diva, wewe elewa tu liko kishkaji, kila mtu ana uhuru wa kufanya mambo yake na haina kubanana, hata hivyo wakati mwingi ninakuwa naye,” alisema Quick Rocka.

Alipoulizwa juu ya tetesi zinazosambaa za Kajala kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Msami alisema hajui chochote kuhusu wawili hao.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com