Hivi karibuni kumeibuka taarifa kuwa ule ukaribu uliokuwepo mwanzo kati ya kundi la Navy Kenzo na Weusi umepotea tangu yalipofanyika mabadiliko ya studio ya The Industry. Nahreel amesema hilo siyo kweli bado ni washkaji kama zamani tofauti watu wanavyowachukulia.

Navy Kenzo na Weusi wamekuwa watu wa karibu sana hali iliyopelekea watu kuona wivu kwa kusema kuwa Nahreel anawapendelea wasanii hao kwa kuwatengenezea beat nzuri zaidi ya wasanii wengine.

Akiongea na Bongo5, Nahreel amesema kuwa wao na Weusi bado ni washkaji na bado wana kazi zao kwenye studio yake hazijatoka.

“Ni kweli utaratibu umebadilika na mimi kama mfanyabiashara mwingine lazima kila siku niendelee kuweka utaratibu fulani,” alisema Nahreel.

“Hapa kati nimekuwa busy na ratiba zangu na focus na Navy Kenzo tumekuwa tuna move hapa na pale kwahiyo unajua Weusi na wao wana mipango yao kama wana muziki siwezi nikawa mimi tu nawacheleweshea time zao, na hapa wana nyimbo nyingi zipo bado hazijatoka,” aliongeza.

Hata hivyo Mei 6 mwaka huu Navy Kenzo walifanya sherehe za kuzindua studio yao ‘The Industry lakini hakuna hata msanii mmoja wa kundi la Weusi aliyehudhuria sherehe hizo.

Chanzo:Bongo5

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com