Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliyofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.

“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.

Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com