Msanii anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amemuumbua upya aliyekuwa mwandani wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa kuanika A-Z ya namna alivyokuwa anamnyanyasa kwenye uhusiano wao wa kimapenzi kiasi cha kuamua kuachana naye. Wikenda limeinyaka.

Akizungumza na Wikienda mara baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya wa Jike Shupa huku ndani yake akigusia kiduchu figisufigisu alizokutana nazo kwenye uhusiano huo akimtumia mrembo anayefanana na Shilole ‘Shilole bandia’.

Nuh aliliambia gazeti hili kuwa alishindwa kustahimili kuacha matukio ya uhusiano wake yapite hivihivi bila kuyagusia kidogo kwenye wimbo wake huo kwa sababu alihisi watu hawamuelewi kile alichokuwa anakisema juu ya Shilole.

“Nimeamua kufanya hivi ili Watanzania waone jinsi Shilole alivyokuwa ananifanyia kupitia mtiririko wa matukio kwenye kichupa changu. Kiukweli inaumiza sana lakini hivyo ndivyo roho yake ilivyo, sijali ataumbuka kwa kiasi gani lakini hizo ni hisia zangu ambazo nimeamua kuziweka upya,” alisema Nuh huku akiongeza kuwa kwa sasa yuko kwenye uhusiano na mwanadada aitwaye Nawal.

Hata hivyo, baada ya gazeti hili kuchonga na Nuh lilimtafuta Shilole ambaye alipoulizwa juu ya sakata hilo alidai kuwa hataki kumzungumzia Nuh wala kusikia habari zake maana hata video yenyewe hawezi kuiangalia.

“Sitaki kusungumzia habari za mtu mwingine, no coment, labda kama kuna ishu nyingine unaweza
kuniambia,” alisema Shilole. Shilole na Nuh waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo mrembo huyo alidai alikuwa akimlea jamaa huyo hivyo Nuh naye ameamua kueleza ukweli namna ambavyo Shilole aligeuka mwanamasumbwi ndani ya nyumba.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com