Ikiwa ni mwezi mmoja na nusu toka rapper Nay wa Mitego aachie video ya wimbo wake ‘Saka Hela’, alhamisi hii amenzaa kushoot video yake mpya ya wimbo ‘Pale Kati Patamu’.

Rapper huyo ameshare picha za maandalizi ya kazi hiyo mpya huku akiwataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi hiyo.

Kupitia instagram, Nay wa Mitego ameandika:
Kama wewe ni shabiki wangu, kaa mkao wa kula tuna kiwasha soon.. #PaleKatiPatamu.
Video ya rapper huyo ya wimbo ‘Saka Hela’ ina view 348,824 katika mtandao wa Youtube toka aiachie Mei Mwaka huu.

Mwezi huyo ni mwezi ambao wasanii wengi wa muziki waliachia video zao mpya akiwemo Shetta ambaye aliachia video ya wimbo wake ‘Namjua’ ambao bado unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya runinga huku Youtube ikiwa na view 963,287.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com