Aliyekuwa mke wa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye pia ni msanii wa filamu, Faiza Ally amefunguka na kueleza kitu ambacho kinamnyima furaha maishani mwake.
Faiza na mtoto wake Sasha

Muigizaji huyo ambaye aliachana na mume wake ambaye ni mbunge Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, amekuwa akilalamika mara kadhaa kuhusu mume wake huyo ambaye alifanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja aitwae Sasha.

“Jambo linalonipa huzuni mara kwa mara ni pale mwanangu Sasha anaponiuliza habari za baba yake, huwa naumia mno. Ila tukio la furaha ambalo siwezi kulisahau ni pale nilipopata uchungu wa dakika kadhaa lakini nilikuja kupata furaha ya maisha yangu yote siku nilipo jifungua, Sasha,” Faiza aliliambia gazeti la Mtanzania.

Hata hivyo, Faiza aliwahi kukaririwa akisema kuwa yupo tayari kuzaa mtoto mwingine na Sugu lakini sio kurudiana naye.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com