MKURUGENZI wa Kituo cha Kusaidia Waathilika wa Dawa Za Kulevya, Sober House, kilichopo Bagamoyo, Pwani, Karim Banji amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amepelekwa katika kituo hicho.

Akizungumza na mtandao huu uliofunga safari mpaka kituoni hapo, Karim alisema kuwa ni kweli siku ya jana (Ijumaa) alipokea taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mwanamuziki huyo kuwa wangempeleka kituoni hapo leo (Jumamosi), lakini hadi majira ya saa tisa leo mchana hakuwa amepelekwa.

“Jana nilipokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni mtu wa karibu wa Ray C (hakumtaja jina) kuwa watamleta leo, hapa unaponiona nimefunga safari kutoka Dar kwa ajili ya suala hilo lakini mpaka sasa hajafika, kama ni kweli watamleta, basi nitawajulisha,” alisema Karim.

Baada ya kupokea maelezo hayo kutoka kwa mkurugenzi huyo, mtandao huu uliacha mawasiliano yake kituoni hapo  na kung’oa nanga kusubiri taarifa zaidi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com