Kwanza nikiri kabisa katika moja ya mtanzania ninaye mkubali Diamond kwa kazi anazozifanya ni mimi apa.Jamaa amekuwa balozi mzuri sana kwa nchi yetu,ameipeperusha vyema bendera katika sekta ya muziki duniani na mengineyo meeeengi ambayo nisijichoshe kuyasema maana mnayafahamu.

Jitihada zake hizi ndizo zimemfanya awe nominated katika tunzo kubwa kabisa za BET kwa mara ya pili.Nasikitika kusema mapema kuwa hatoweza kushinda iyo tunzo kwa mwaka huu labda achaguliwe tena kwa mara ya tatu mwakani.

Nimesema hatoweza kuchukua mara baada ya kuangalia mwenendo wa mpinzani wake mkubwa kwenye tunzo hii WIZKID WIZKID WIZKID!!!!!! Daah huyu dogo kwasasa anatrend mnoo marekani kuliko hata afrika,naweza kusema amefaulu kupenyeza mziki wake marekani kwa 55%.
Hii ni mara tu alipofanya colabo na Drake ,wimbo uliomfungulia njia mara baada ya wimbo huitwao 'one dance' kuvunja rekodi kwenye billboard top 100.Juzikati hapo pia aliperform colabo yake nyingine aliyofanya na Chriss Brown wimbo wao unaitwa 'African bad girl'..hili nalo ni bonge la hit...hakuishia hapo,nyota ikazidi kung'ara kwake mara baada ya kupost picha akiwa na super producer wa marekani Swizz Beatz na kuweka caption ya kuashiria kuna hit nyingine inakuja...

Kwa mwendo huu naona ni vigumu sana kijana wetu Diamond kuchukua tunzo ya BET kwasasa maana mbabe wake Wizkid tayari kashawasha moto huko Marekani na watu washamkubali...naweza kusema ''Diamond wa kimataifa,lakini Wizkid wa kidua"

All in all tumtakie tu kila la kheri mtanzania wetu na kumuombea pia..namshauri Mondi akishatoa kolabo ya Psquare, hit inayofatia atoe aliyofanya na Wizkid kwanza kabla ya ile aliyofanya na Neyo...maana ni ukweli usiopingika kwasasa Marekani wanamsikiliza zaidi Wizkid kuliko wanavomsikiliza Neyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com