Huku kukiwa na madai ya ndoa ya staa wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na mwigizaji Flora Mvungi kusambaratika, mwana mama huyo amedaiwa kurudi nyumbani kwa mama yake mzazi, Kimara jijini Dar.

Awali, mtoa taarifa wetu ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo, amedokeza kuwa chanzo cha Flora kurudi kwao Kimara ni mzozo uliotokea katika hoteli moja iliyopo Magomeni Mwembechai (jina linahifadhiwa).

H.Baba-akiwa-na-mke-wake-Frora-MvungiH.Baba akiwa na mke wake Frora Mvungi
“Mzozo ulikuwa mkubwa siyo kitoto, mastaa wote wanajua, wanajitahidi kuwasuluhisha ili suala lisifike magazetini. Flora alitoa picha zote za mumewe, lakini mama (anatajwa jina mdau mkubwa wa filamu, ambaye hakupatikana) akamshauri arudishe picha hizo ili watu wasishtukie, ndo anaweka kwa shingo upande lakini kwa sasa Flora yupo nyumbani kwao Kimara na H. Baba ametimkia Mwanza,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa H. Baba kwa njia ya simu, alikiri kuwa yupo Mwanza na mkewe yupo kwao Kimara lakini hakuna mzozo wowote kati yao.

Alisema hashangazwi na habari hizo kwa sababu siku zote watu wamekuwa wakimuombea mabaya katika ndoa yake, kwanza walianza hivyo tangu walipooana wakidai wasingeweza kufikisha mwaka mmoja wakiwa pamoja.

“Kuna watu wanatuombea mabaya tangu zamani, sisi tupo imara na hakuna wa kututenganisha isipokuwa Mwenyezi Mungu,” alisema H. Baba na kuongeza kuwa;

“Mke wangu kweli yupo kwao kwa sababu kila nikisafiri yeye huenda huko ambapo hukaa wiki au zaidi na ninaporudi naye hurejea. Ameenda na watoto wote na kule nyumbani kwangu wapo wadogo zangu.”

Chanzo:Global Publishers

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com