Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Telecommunication engineering.

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.

“Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Telecommunication engineering,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com