Habari ‘hot’ iliyotua kwenye meza ya gazeti hili inadai kuwa lile penzi lililokuwa gumzo mjini kati ya Mwanamuziki Kalala Hamza ‘Junior’ na msanii wa filamu za Kibongo, Rose Alphonce ‘Muna Love’ limevunjika na sasa jamaa huyo amehamishia majeshi kwa mwigizaji aitwaye Mamy Mushi.

Inaelezwa kuwa, sasa hivi Kalala na Mamy wamekuwa ni kama kumbikumbi kwani wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali za kujiachia.Akizungumzia kumwagana na Kalala, Muna alisema kwa kifupi: “Ni kweli nimeachana na Kalala. Sasa kila mmoja ana maisha yake.”


Kalala ambaye kwa sasa anapiga mzigo kwenye Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ hakupatikana kuzungumzia penzi lake jipya ila Mamy alipozungumza na Ijumaa alikiri kumrithi Muna: “Penzi letu wala siyo la kificho, Muna na Kalala ilikuwa zamani, sasa ni zamu yangu.”

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com