Familia ya staa wa Bongo Fleva, Juma Musa ‘Jux’ imeingilia kati ishu ya mwanaume ‘tata’, mkazi wa Dar, James Delicious aliyetangaza kumtaka kimapenzi msanii huyo ambaye ni mpenzi wa Mwanamuziki Vanessa Mdee ‘V-Money’.

Akizungumza na Wikienda kwa niaba ya familia, dada wa Jux, Fatu-ma Juma alisema kuwa hakuna kitu kinachowaudhi kama kijana huyo kutwa kutangaza kumpenda na kumtaka mdogo wao huyo wakati wote ni wanaume na ni kinyume cha maadili ya kidini (familia ya Kiislam), Kitanzania na Kiafrika kwa jumla.

“Kiukweli familia inachukizwa sana na tabia ya huyo kijana ambaye haoni aibu, tunamtaka kuacha mara moja kusumbua watu akitaka namba ya Jux la sivyo tutachukua hatua za kisheria kwani anatukera sana,” alisema Fatuma.

Hivi karibuni kijana huyo alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa lazima ampindue Vanessa kwa Jux kwani anampenda jamaa huyo kupita kiasi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com