Mshindi wa Oscar na raia wa nchini Kenya ‘Lupita Nyong’o’ anatarajiwa kuigiza na kutengeneza filamu ya mwandishi wa novel ambae ni raia wa nchini Nigeria ‘Chimamanda Ngozi Adichie’ kwenye filamu inayotarajiwa kuitwa ‘Americanah’. Filamu hiyo ambayo itatengenezwa na kampuni ya ‘Plan B’ ya Actor, Director na Producer ‘Brad Pitt’ ambayo pia ilitengeneza filamu ya ’12 Years a Slave’ iliyompa sifa nyingi mwanadada huyo.
Americanah inahusu wanigeria wawili ambao walipendana sana, ila wakajikuta wametengana kwasababu ya mambo ya uhamishaji.
Nyong’o amesema kwamba anafuraha kubwa kuigiza kitabu cha ‘Ms Adichie’s’ kwenye screen. Americanah inahusu wapendanao wawili ‘Ifemelu’ na ‘Obinze’ ambao walishinda kwenye ‘US National Book Critics Circle Award’ mwaka 2013, ambapo kitabu hicho Kilichaguliwa kwenye vitabu 10 bora kwenye “New York Times Book Review” na kujipatia umaarufu sana katika dunia ya vitabu na sasa ipo mbioni kuonekana kwenye Screen.
-BongoSwaggz

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com