Kampuni ya MultiChoice Africa inayoandaa mashindano ya Big Brother Africa imetangaza tarehe ya usaili wa shindano hilo mwaka huu katika nchi mbalimbali za Afrika.
Waandaaji hao wameitaja nchi ya Rwanda mwaka huu kuwa miongoni mwa nchi zitakazokuwa na washiriki katika shindano hilo mwaka huu ambapo mshindi ataondoka na kibunda cha $300,00.
Nchi zitakazoshiriki mwaka huu ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika Kusini, Sierra Leone, Nigeria, Botwasana, Malawi, Namibia, Ghana, Zimbabwe na Ethiopia.
Kwa Tanzania, usaili utafanyika July 11 na July 12 jijini Dar es Salaam (New Africa Hotel).
Ni muda wa kuona sarakasi nyingine na kuibua mengi mapya yakiwemo mahusiano ambayo mengine huwa na nguvu hata baada ya kumalizika kwa shindano hilo.
Mwaka jana mshiriki wa Namibia, Dillish Mathews aliibuka mshindi wa msimu huo ulipewa jina la The Chase. 
KWA KUPATA STORY NA MAPICHA ZAIDI BOFYA HAPA
-tanzanianewz

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com