Staa wa kike wa filamu za kibongo, Jackline Wolper amefunguka kuwa kwa sasa hana wazo kabisa la kubeba mimba kwani staili ya kifo cha Recho Haule inamuumiza sana kichwa....
Ingawa Wolper anaamini kuwa ni wajibu wa kila mwanamke kuzaa, lakini aina ya kifo ambacho rafiki yake kipenzi Recho amekufa nacho kimekuwa ikimtesa sana moyoni na kumfanya afute mipango yake ya kuzaa akihofia kufa.
"Najua ni wajibu wetu kuzaa, lakini nimekuwa na hofu kubwa ya kushika mimba sababu mimi ni muoga sana wa kuzaa, na kila nikikumbuka kifo cha Recho ndo kabisaa nazidi kuchanganyikiwa.
"Napenda sana kuwa na mtoto, lakini si leo wala kesho. Nahitaji muda wa kujenga ujasiri mpya, lakini kama itatokea ntajitahidi kuvumilia,"alisema 
KWA PICHA NA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com